Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Jedwali linaonesha kuwa, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2023 umefika asilimia 3.6 kutoka asilimia 4.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2023.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 108.93 mwezi Juni, 2022 hadi 112.81 mwezi Juni, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Juni,2023.