Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2024 umebaki katika asilimia 3.0 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2024.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2024 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2024. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 112.13 mwezi Machi, 2023 hadi 115.51 mwezi Machi, 2024.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Machi,2024(pdf)