Kijitabu cha Takwimu za Msingi cha Tanzania mwaka 2022 kinatoa picha ya hali halisi ya mwenendo katika nyanja za uchumi, jamii, mazingira na siasa. Kitabu hiki kinawasilisha mtiririko wa takwimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.

Kijitabu hiki kina takwimu kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa kutoka machapisho ya takwimu rasmi yanatolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara, Idara na Wakala nyingine za Serikali. Taarifa za takwimu zilizowasilishwa ni muhimu kwa kupanga mipango, kufuatilia na kutathimini programu mbalimbali za maendeleo katika ngazi zote za kiutawala.