SG Dkt. Msengwa: Takwimu za Tabianchi Hazipaswi Kuishia katika Wastani wa Kitaifa Pekee
Bali zinapaswa kutueleza nani anaathirika, anaathirika wapi, anaathirika kwa namna gani, na kwa nini athari za mabadiliko ya tabianchi zinatofautiana kati ya jamii na makundi mbalimbali ya watu. Dkt. Msengwwa ameyasema hayo tarehe 02 Septemba 2026 wakati akifunga warsha ya kitaifa kuhusu upatikanaji wa Takwimu za kupima mabadiliko ya Tabianchi nchini.