Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2019 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2019. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2019 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2019. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 116.82 mwezi Aprili, 2019 kutoka 113.20 mwezi Aprili, 2018.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi April ,2019