Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2020 umebaki kuwa asilimia 3.1 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 119.43 mwezi Oktoba, 2020 kutoka 115.84 mwezi Oktoba, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba 2020