Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.6 kutoka asilimia 4.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 103.80 mwezi Agosti, 2021 hadi 108.63 mwezi Agosti, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Agosti,2022.