Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 umeongezeka hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2022. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 105.59 mwezi Januari, 2022 hadi 110.81 mwezi Januari, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Januari,2023.