Pato la Taifa katika Robo ya Pili (Aprili - Juni) mwaka 2023, kwa bei za mwaka husika liliongezeka hadi Shilingi trilioni 47.6 kutoka Shilingi trilioni 42.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Aidha, Katika kipindi hicho, Pato Halisi la Taifa (bei za mwaka wa kizio 2015) liliongezeka hadi Shilingi trilioni 36.7, kutoka Shilingi trilioni 34.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2022, sawa na ukuaji wa asilimia 5.2.

Kupakua taarifa hii bofya hapa