Vifo vinavyotokana na uzazi vinajumuisha, vifo vya akina mama wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua na ndani ya siku 42 baada ya kujifungua bila kujumuisha vifo vilivyotokana na ajali au ukatili wa majumbani.

Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022 nchini Tanzania (TDHS-MIS 2022) yanaonesha kuwa vifo vinavyotokana na uzazi (MMR) kwa Tanzania ni vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa kipindi cha miaka saba kabla ya utafiti. Kiwango cha uhakika wa idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi kwa mujibu wa utafiti wa TDHS-MIS 2022 ni kati ya vifo 59 hadi 149 kwa kila vizazi hai 100,000.

Bonyeza hapa kupakua taarifa zaidi