Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2020 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2020. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.20 mwezi Machi, 2020 kutoka 116.23 mwezi Machi, 2019.      

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Machi 2020