Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2020 umeongezeka hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2020 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.79 mwezi Desemba, 2020 kutoka 117.10 mwezi Desemba, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba 2020