Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2021 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 100.49 mwezi Julai, 2020 hadi 104.32 mwezi Julai, 2021.     

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Julai, 2021