Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2021 umebaki kuwa asilimia 3.8 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2021. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2021 iko sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 99.96 mwezi Agosti, 2020 hadi 103.80 mwezi Agosti, 2021.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Agosti, 2021