Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021 umebaki kuwa asilimia 4.0 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2021. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 99.59 Oktoba, 2020 hadi 103.61 mwezi Oktoba, 2021.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba,2021