Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Jedwali Namba 1 linaonesha kuwa, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2022 umepungua kidogo hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2022. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2022 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 103.41 mwezi Machi, 2021 hadi 107.09 mwezi Machi, 2022.


Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Machi,2022