Pato la Taifa katika robo ya nne (Oktoba - Desemba) ya mwaka 2019, kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi shilingi trilioni 39.1 ikilinganishwa na shilingi trilioni 34.5 katika robo ya nne ya mwaka 2018. Vile vile, thamani ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka wa kizio wa 2015 iliongezeka hadi shilingi trilioni 33.7 katika robo ya nne ya mwaka 2019 kutoka shilingi trilioni 31.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2018, sawa na ukuaji wa asilimia 7.0.

Bofya hapa Kupakua Muhtasari wa Pato la Taifa Robo ya Nne mwaka 2019 (pdf)

Bofya hapa Kupakua Muhtasari wa Pato la Taifa Robo ya Nne mwaka 2019 (Excel)