Thamani ya Pato la Taifa katika robo ya pili (Aprili - Juni) mwaka 2020 kwa bei za miaka husika iliongezeka hadi shilingi trilioni 37.6 kutoka shilingi trilioni 34.9 katika katika kipindi kama hicho mwaka 2019. Aidha, katika kipindi hicho, thamani ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 iliongezeka hadi shilingi trilioni 32.0 mwaka 2020 kutoka shilingi trilioni 30.7 mwaka 2019 sawa na ukuaji wa uchumi wa asilimia 4.0.

Kusoma zaidi bonyeza hapa