Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Orodha ya Shughuli za Kiuchumi na Kijamii

Sensa kwa ajili ya orodha ya shughuli za kiuchumi na kijamii inajumuisha uorodheshaji na ukusanya taarifa kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii zinazofanya kazi katika jengo au majengo ya kudumu ndani ya mipaka ya nchi. Kwa kawaida sensa hii hufanyika kwa kufuata mwongozo wa kimataifa wa uorodheshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii (ISIC REV4) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya sensa na kutoa ripoti ya pamoja inayojumuisha taarifa za shughuli za kiuchumi na kijamii za Tanzania Bara na Zanzibar kwa mwaka 2023/2024. Lengo kuu la sensa hii ni kupata orodha ya shughuli za kiuchumi na kijamii katika sekta rasmi nchini ambayo itatumika kama muhimili wa sampuli kwa ajili ya tafiti mbalimbali za kiuchumi na kijamii.