DCP Kaziulaya Atembelea Maktaba ya NBS Dodoma
DCP Kaziulaya Atembelea Maktaba ya NBS Dodoma
Posted On: 23 January, 2026
Naibu Kamishna wa Magereza Makao Makuu Dodoma, DCP Justin Kaziulaya ametembelea Maktaba ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyopo Makao Makuu ya Ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 22 Januari 2026.
Pamoja na mambo mengine, DCP Kaziulaya ameridhishwa na namna Maktaba hiyo inavyofanya kazi ambapo Mkutubi, Issa Bernard Magabiro amemkabidhi machapisho ya Takwimu mbalimbali kwa ajili ya kupanga na kufanya maamuzi ya shughuli za kila siku za Jeshi hilo.