Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Majukumu na Huduma

MAJUKUMU

Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu, Sura 351, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imepewa jukumu la kuzalisha, kuratibu, kusimamia, kusambaza na kuhifadhi takwimu rasmi nchini. Katika kutekeleza jukumu hilo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inatakiwa kufanya yafuatayo;

  1. Kuendesha Sensa ya Watu na Makazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar;
  2. Kuishauri Serikali na umma kwa ujumla kuhusu masuala ya takwimu rasmi;
  3. Kutoa takwimu rasmi za kuaminika na zenye ubora wa hali ya juu kwa umma;
  4. Kuanzisha  na kusimamia kituo cha kuhifadhi ripoti za takwimu rasmi, machapisho, nyaraka na data kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  5. Kuandaa mbinu, viwango, dhana na maana za kitakwimu kwa ajili ya uzalishaji wa takwimu rasmi;
  6. Kudhibiti/kusimamia takwimu rasmi;
  7. Kuratibu usambazaji wa taarifa za kitakwimu;
  8. Kuratibu na kusimamia Mfumo wa kitaifa wa Takwimu nchini; na
  9. Kutekeleza majukumu yote muhimu au yanayohitajika kwa madhumuni ya ofisi chini ya Sheria ya Takwimu. 

 

HUDUMA NYINGINE

Pamoja na majukumu hayo Ofisi ya Taifa ya Takwimu, inatoa huduma zikiwemo zifuatazo:

  1. Huduma za ushauri wa kitakwimu;
  2. Kutayarisha sampuli za tafiti;
  3. Orodha ya maeneo yote nchini yanayotumika kuchagua maeneo sampuli ya kuhesabia;
  4. Kutoa ramani za maeneo ya utafiti (Enumeration Area (EA) maps);
  5. Kazi za Kitakwimu kwa matakwa ya mteja kwa malipo;
  6. Huduma za Maktaba; na
  7. Huduma za kumbi za mikutano.