Tanzania Integrated Statistical Portal (TISP)
TISP ni mfumo jumuishi wa Takwimu unaounganisha mifumo mbalimbali ya Kitakwimu ili kuwa na dirisha moja la takwimu lenye ubora kutoka taasisi za serikali kwa sekta kama Afya, maji, Elimu n.k. TISP ina dashibodi na moduli mbalimbali kama Dashibodi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG), Dashibodi ya Sensa, moduli ya Utafiti wa Afya (DHS) na Mfumo wa Kuonyesha Majedwali ya Takwimu (TASIS) inawezesha upatikanaji wa taarifa kwa wakati. Kupitia TISP, pamoja na kuhuisha taarifa za kiutawala(administrative). Ofisi ya Taifa ya Takwimu inahakikisha kuwa taarifa za sensa na tafiti mbalimbali zinapatikana kwa urahisi zkwa kutumia teknolojia za kisasa. Mfumo huu unalenga kuboresha mipango, bajeti, na maamuzi yenye msingi wa ushahidi, huku ukichangia maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi kwa kiwango cha kitaifa na kimataifa.