SG, Dkt. Msengwa Awasilisha Ripoti ya Uwezeshaji Wanawake, Lishe WMJJWMM
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa, amewasilisha Ripoti ya Utafiti wa Uwezeshaji Wanawake na Lishe - WEN kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (WMJJWMM), Dkt. John Jingu kupitia kikao maalum kilichofanyika ofisini kwa katibu Mkuu huyo Mtumba jijini Dodoma mapema leo tarehe 22 Januari 2026.
Aidha, Dkt. Msengwa amefafanua kwa kina umuhimu wa Takwimu za Jinsia na namna uwezeshaji wa Wanawake unavyoweza kuingiliana na ubora wa Lishe.
Akiwasilisha Ripoti hiyo Mratibu wa Utafiti huo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Samweli Kawa amesema lengo la Utafiti huo ni kupata Takwimu kuhusu uwezeshaji Wanawake na lishe ili kuboresha huduma za lishe katika ngazi ya kaya, familia na Jamii.
Wasilisho hilo limefanyika mbele ya Menejimenti ya Wizara hiyo.