The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics Tanzania

Statistics for Development
Tuzo
Posted On: 25 August, 2025
Tuzo

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Amina Msengwa na Wasaidizi wake wakiwa na Tuzo baada ya Ofisi ya Taifa ya Takwmimu NBS kushinda nafasi ya Pili katika Ubora wa Uandaaji wa Taarifa na Usimamizi wa Fedha (Best Financial Management Performance) kwa Taasisi za Umma zisizo za Kibiashara (Non Commercial Entity) kwa mwaka 2025.

Tuzo hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa hazina na kukabidhiwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mtakwimu Mkuu wa Serikali tarehe 24 Agosti,2025 katika Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za umma Jijini Arusha.