FUNGUA KWA MAONI - MAANDALIZI ya Sensa ya Uzalishaji Viwandani 2023
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inajiandaa kufanya Sensa ya Uzalishaji wa Viwandani kwa mwaka wa rejea 2023 itakayohusisha shughuli nne za kiuchumi kama ilivyoainishwa kwenye mgawanyo wa shughuli za kiuchumi (ISIC Rev. 4) ambazo ni Uchimbaji wa Madini na Kokoto; Utengenezaji wa bidhaa viwandani; Uzalishaji na usambazaji wa umeme, gesi, mvuke na ubadilishaji wa hali joto au baridi na Usambazaji maji; mifumo ya maji taka, udhibiti wa taka na shughuli za urejeshaji. Sensa ya Uzalishaji Viwandani itatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar na wadau wengine muhimu wa kisekta.
Lengo la Sensa ya uzalishaji Viwandani ni kupata taarifa za viwanda kuendana na wakati zitakazosaidia kupima mchango wa sekta katika uchumi nchini pamoja na kupata mhimili wa sampuli kwa ajili ya tafiti nyingine , uchambuzi wa mipango na utungaji wa sera unaoendana na ushahidi wa kitakwimu pamoja na kufanya maamuzi.
Kwa maoni/mchango kuhusu maudhui ya madodoso ya sensa, tafadhali pakua hapa chini.