Fahirisi za Bei za Biashara (TPI)
Fahirisi za Bei za Biashara (TPI)
Fahirisi za bei za biashara ni viashiria vya kiuchumi vinavyotumika kupima wastani wa mabadiliko ya bei za bidhaa zilizouzwa katika kipindi husika. Viashiria hivi ni muhimu katika kufahamu mwelekeo wa biashara na mfumuko wa bei za bidhaa zilizouzwa na kununuliwa katika uchumi. Fahirisi za bei za biashara zimeainishwa katika makundi ya bidhaa zilizouzwa nje na bidhaa zilizoagizwa kutoka nje. Fahirisi za bei za bidhaa zilizouzwa nje hupima mabadiliko ya bei za bidhaa zilizouzwa nje kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi, wakati fahirisi za bei za bidhaa zilizonunuliwa kutoka nje hupima mabadiliko ya bei kutoka kwa wauzaji wa nje ya nchi.