Takwimu za Biashara za Nje
Ripoti ya Takwimu za Biashara ya Nje inatoa muhtasari ya biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine duniani na kikanda, ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Sehemu hii pia inajumuisha fahirisi za bidhaa zinazouzwa na kuagizwa kutoka nje ya nchi yaani Trade Price Indices (TPI) ambavyo ni viashiria muhimu vya kiuchumi vinavyotumika kupima mabadiliko ya wastani ya bei za bidhaa zinazouzwa na kununuliwa kwa kipindi husika. Fahirisi hizi zina mchango mkubwa katika kuchambua mwenendo wa biashara na kutoa viashiria vya mfumuko wa bei katika uchumi. Kwa maelezo zaidi, wasiliana kwa Barua pepe: valerian.tesha@nbs.go.tz