Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto (TDHS)
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022 (TDHS-MIS) ni utafiti wa Saba (7) kufanyika nchini Tanzania kupitia programu ya DHS. Utafiti huu umefanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS), Zanzibar na Wizara za Afya (MOH) kutoka Bara na Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali na wadau wa maendeleo. Shirika la ICF lilitoa msaada wa kiufundi kupitia programu ya DHS katika utekelezaji wa Utafiti wa huu.
Lengo kuu la Utafiti wa TDHS/MIS wa Mwaka 2022 ni kupata taarifa za sasa za afya na takwimu mbalimbali zinazohusiana na masuala ya afya ili kusaidia kuboresha sera katika ajenda ya maendeleo ya Kimataifa, kitaifa, kikanda na kimataifa.
Taarifa hii ni muhimu sana kwa watunga sera, mameneja wa programu mbalimbali na wadau wengine wanapofanya maamuzi mbali mbali hususan katika sekta ya afya kwa kutumia Ushahidi wa Kitakwimu.