Takwimu za Afya
Takwimu za afya zinajumuisha aina mbalimbali za takwimu. Takwimu zinazotolewa mara nyingi ni pamoja na takwimu muhimu za matukio ya binadamu (vizazi, vifo, ndoa na talaka), Magonjwa (kiwango cha maambukizi mapya ya ugonjwa katika jamii) na Vifo (idadi ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa fulani ikilinganishwa na jumla ya idadi ya watu). Takwimu nyingine zinazotolewa ni gharama za huduma za afya, mgawanyo wa magonjwa kidemographia kwa kufuata maeneo ya kijiographia, jinsia na takwimu za hali ya kijamii na kiuchumi. Utoaji wa takwimu za afya ni moja ya majukumu muhimu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Yafuatayo ni machapisho yanayotokana na takwimu za afya yanayotolewa na kusambazwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.