Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Fahirisi za Uzalishaji Viwandani (IIP)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutayarisha fahirisi za uzalishaji wa bidhaa viwandani kila robo mwaka. Fahirisi za uzalishaji wa bidhaa viwandani hupima mabadiliko ya kiasi cha bidhaa zilizozalishwa kwa aina ya sekta ya viwanda katika uchumi. Fahirisi hii huonesha utekelezaji wa sekta za viwanda. Vilevile, fahirisi hii huonesha  mabadiliko ya kiasi cha uzalishaji wa bidhaa katika vipindi vifupi vifupi kwa lengo la kubainisha athari zake katika hatua za awali, hivyo kuwezesha kufanya uamuzi wa kisera katika wakati muafaka na pia kufanya maoteo ya utekelezaji wa shughuli ya uzalishaji viwandani.

Takwimu za uzalishai wa bidhaa viwandani hukusanywa kila robo mwaka. Robo mwaka zinazohusika ni : robo ya Kwanza: Januari – Machi; robo ya Pili: Aprili – Juni; robo ya Tatu: Julai – Septemba; na robo ya Nne: Oktoba – Desemba.