Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Takwimu za Viwanda za Mwaka

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara (MIT) hufanya Utafiti wa Uzalishaji Viwandani kwa Mwaka (ASIP). Lengo kuu la Utafiti wa kila mwaka wa Uzalishaji Viwandani ni kutoa taarifa sahihi zinazohusu sekta ya viwanda ambazo zinatumika katika kutathmini mchango wa sekta ya viwanda kwa uchumi wa Nchi. Aidha, unalenga kutoa taarifa za msingi ambazo zanatumika kufanikisha tafiti nyingine na kuwezesha uchambuzi wa mipango mbalimbali, utungaji wa sera kwa msingi wa ushahidi na kusaidia katika kufanya maamuzi sahihi.