Jukwaa la Kitaifa la Tathmini ya Takwimu za Afya za Lishe (NEP)
Jukwaa la Kitaifa la Tathmini ya Takwimu za Afya za Lishe (NEP)
NEP ni mbinu mpya madhubuti ya kukusanya na kuchambua data za afya na lishe kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ili Serikali ipate majibu ya kimkakati na yanayotegemea ushahidi wa kitakwimu kwa maswali muhimu zaidi kuhusu programu na sera za Afya ya Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, na Lishe (MNCH&N).
NEP inajumuisha mkusanyiko wa zana zinazosaidia watunga maamuzi kufafanua maswali kipaumbele ya tathmini, kupanga na kusimamia takwimu, kutathmini ubora wa takwimu, kuchambua takwimu na kuwasilisha matokeo. Tanzania inatekeleza mradi wa NEP kati ya mwaka 2014-2017 kwa msaada wa ufadhili kutoka Serikali ya Canada na Mwongozo wa kiufundi pamoja na msaada wa kujengewa uwezo kutoka Taasisi ya Programu za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Johns Hopkins (IIP-JHU).