Utafiti wa Kufuatilia Kaya (NPS)
Utafiti wa Kufuatilia Kaya Tanzania ni utafiti wa ngazi ya kaya wenye uwakilishi wa kitaifa unaokusanya taarifa zinazohusiana na maisha ya watu ikiwemo matumizi, uzalishaji katika kilimo na shughulli nyingine za kipato zisizo za kilimo na takwimu za kijamii na kiuchumi. Utafiti huu unajumuisha viashiria mbalimbali vya kiuchumi, kijamii, na mazingira na hukusanya taarifa kutoka katika kaya zile zile zilizohojiwa tangu kuanza kwa utafiti ili kuweza kufuatilia viashiria hivi vya kimaendeleo vya kitaifa na kimataifa, kupima kwa uhalisia kiwango halisi cha mabadiliko katika viashiria vya umaskini, kubaini uhusiano uliopo baina ya wakulima wadogo na ustawi wao, na kutathmini sera na mipango iliyopo nchini Tanzania. Tangu kuanza kwa utafiti huu mnamo mwaka 2008/2009, jumla ya tafiti tano (5) zimeshafanyika.