Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Viashiria vya Umasikini

Takwimu za viashiria vya umaskini husaidia kubaini katika jamii ni nani maskini, wanaishi wapi na vigezo vinavyopelekea kaya kuwa maskini ikilinganishwa na kaya nyingine katika jamii ile ambazo huonekana kuwa katika hali bora. Lengo la uchambuzi wa takwimu za viashiria vya umaskini ni kuwa na uwezo wa kuandaa mikakati mahsusi kwa ajili ya kupunguza au kuondoa umaskini inayolenga maskini, ambayo itasaidia kuelewa ni kwa nini wengine katika jamii ni maskini na wengine wana hali bora. Utoaji wa takwimu za viashiria vya umaskini ni moja ya majukumu muhimu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Yafuatayo ni machapisho yanayotokana na takwimu za viashiria vya umaskini yanayotolewa na kusambazwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.