Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Fahirisi za Bei za Mzalishaji (PPI)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutayarisha fahirisi za bei za mzalishaji wa bidhaa kila robo mwaka. Fahirisi za bei za mzalishaji wa bidhaa hupima wastani wa mabadiliko ya bei za bidhaa ambazo baadhi ya wazalishaji wa bidhaa waliochaguliwa katika soko la ndani hupokea kama malipo ya bidhaa walizozalishaji.

Bei za bidhaa zilizochaguliwa hukusanywa kila robo mwaka. Bei za wazalishaji wa bidhaa hukusanywa tarehe 15 ya kila mwezi katika robo mwaka husika. Robo mwaka zinazohusika ni : robo ya Kwanza: Januari – Machi; robo ya Pili: Aprili – Juni; robo ya Tatu: Julai – Septemba; na robo ya Nne: Oktoba – Desemba.