Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Utafiti wa Tathmini ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Shule (SWASH)

Utafiti wa Tathmini ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shule/Skuli wa Mwaka 2018 ulitekelezwa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) na Ofisi ya Mkuu wa Takwimu za Serikali (OCGS) Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST); Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar (MoEVT); Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PO-RALG); na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum (PO-RALGSD), Zanzibar. Utafiti huu ni wa kwanza kufanyika nchini na umetoa matokeo katika ngazi ya Kitaifa, kwa shule za msingi na sekondari.

Utafiti huu pia ulilenga kutoa taarifa zinazohusu hali ya upatikanaji wa maji safi ya kunywa, huduma za vyoo na usafi wa mazingira nchini Tanzania.

Matokeo ya utafiti huu yatatumika kuthibitisha na kuongeza kanzidata ya takwimu zinazokusanywa na wizara kutoka mashuleni kuhusiana na huduma za maji, elimu ya afya na usafi wa mazingira.