Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania (THMIS)
Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania (THMIS)
Tafiti za Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania (THMIS) zilitekelezwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali – Zanzibar (OCGS-Zanzibar). Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Zanzibar (ZAC) zilitoa idhini ya kufanyika kwa utafiti hizi. Utafiti hizi zilifadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID), TACAIDS, na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (MoHSW). ICF International ilisaidia kufanyika kwa utafiti huu kupitia mradi wa MEASURE DHS unaofadhiliwa na USAID. Mradi wa MEASURE DHS unatoa msaada wa kiufundi na fedha kwa tafiti za demografia na afya katika nchi mbalimbali duniani.