Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania

Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2022-2023 ni utafiti wa kitaifa unaofanyika katika ngazi ya kaya kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi ili kupima athari za maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kitaifa na kimkoa. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ya Tanzania Bara na Tume ya kudhibiti UKIMWI, Zanzibar (ZAC), Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimesimamia Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania (THIS 2022-2023). Utafiti huu umeratibiwa na kutekelezwa kwa pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS) na msaada wa kiufundi umetolewa na Taasisi ya Kukinga na Kudhibiti Magonjwa ya Marekani (CDC) na Taasisi ya ICAP ya Chuo Kikuu cha Columbia.