NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

Inflation Rate for June, 2026: 4.0% AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

Kamati ya Uongozi MoF Yapitia Utekelezaji Mradi wa TSMP II, Kupitisha Bajeti Mwaka wa Fedha 2026/2027
15 July, 2026
10:00:00 - 13:30:00
Hazina
sg@nbs.go.tz

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini (TSMP II), Dkt. Natu El-maamry Mwamba ameongoza kikao cha nne cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 15 Julai 2026, kupitia utekelezaji wa shughuli za Mradi huo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26.

Imeelezwa kuwa utekelezaji wa Mradi huo unaridhisha kwa kuwa mpaka sasa umefikia asilimia 88.9 ya utekelezaji wake tangu uanze kutekelezwa mwaka 2022/23 na utafikia tamati Mwezi Juni 2027.

Vilevile, kupitia kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo mdogo wa mikutano Jengo la Hazina Dodoma, Kamati hiyo ilipitia na kupitisha mpango kazi pamoja na Bajeti ya Mwaka 2026/27 ambapo Mwenyekiti na Wajumbe walizielekeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu – NBS na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar – kushirikiana kwa pamoja na watekelezaji wengine katika Mfumo wa Taifa wa Takwimu nchini kujituma zaidi ili kufikia malengo ya Mradi huo katika kipindi kilichobaki.

Kamati ya Uongozi MoF Yapitia Utekelezaji Mradi wa TSMP II, Kupitisha Bajeti Mwaka wa Fedha 2026/2027