The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

Statistics for Development
UTAFITI WA KUFUATILIA KAYA TANZANIA (NPS) WA MWAKA WA 6

UTAFITI WA KUFUATILIA KAYA TANZANIA (NPS) WA MWAKA WA 6

 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ipo katika maandalizi ya Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6 – NPS 2026). Lengo la utafiti ni kukusanya taarifa mbalimbali za kufuatilia hali ya umaskini na viashiria vingine katika ngazi ya kaya kama vilivyoainishwa katika mipango mbalimbali ya Serikali na ile ya Kimataifa. Utafiti huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2008/09.

NBS inawasilisha madodoso yatakayotumika katika utafiti ili kupokea maoni kutoka kwa wadau. Mwisho wa kupokea maoni ni tarehe 27 Februari 2026 na baada ya kupokea maoni kutakuwa na kikao cha wadau mnamo wiki ya kwanza ya mwezi Machi.

Kwa maoni tuma email: jocelyn.rwehumbiza@nbs.go.tz