NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026 Tanzania Inflation Rate April 2026: 4.0 %
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

NBS, OCGS Zaanza Uhakiki, Uchambuzi wa Taarifa Utafiti wa Sekta Isiyo Rasmi 2025
Posted On: 13 May, 2026
NBS, OCGS Zaanza Uhakiki, Uchambuzi wa Taarifa Utafiti wa Sekta Isiyo Rasmi 2025

Ofisi ya Taifa ya Takwimu – NBS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar - OCGS zimeanza uhakiki na uchambuzi wa taarifa za Utafiti wa Sekta Isiyo Rasmi wa mwaka 2025 kwa lengo la kupata takwimu bora zitakazoisaidia Serikali pamoja na wadau kupanga mipango ya maendeleo nchini hususan uratibu wa biashara zilizo kwenye sekta isiyo rasmi.

Wataalam wa NBS na OCGS wapo mkoani Kigoma kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 24 Mei 2025 kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

Akizungumza katika zoezi hilo ambalo linafanyika katika Ofisi ya Takwimu ya Mkoa wa Kigoma, Kaimu Meneja wa Idara ya Ajira na Bei, Hashim Njowele, amesema kuwa lengo kubwa la Utafiti huo ni kufahamu hali ya sekta isiyo rasmi nchini pamoja na kupata taarifa zinazotumika kuratibu mipango mbalimbali ya Serikali, ikiwemo kurasimisha sekta hiyo ili iweze kuchangia zaidi katika uchumi wa Taifa.

Njowele amesema kuwa timu ya utafiti huo ipo mkoani Kigoma kwa ajili ya kufanya uchambuzi na uhariri wa taarifa zilizo kusanywa wakati wa zoezi la Utafiti, ikiwa ni hatua muhimu kabla ya maandalizi ya ripoti ya Utafiti na kutanganzwa kwa matokea rasmi ya Utafiti huo.

Ameeleza kuwa mnyororo wa kufanya utafiti una hatua mbalimbali ambapo hatua ya kwanza ni maandalizi, hatua ya pili ni ukusanyaji wa taarifa uwandani, hatua ya tatu ni uhariri na uchambuzi wa taarifa na hatua ya mwisho ni uandishi wa ripoti na kutangaza matokeo.

Kwa upande wake Mtakwimu Mwandamizi ambaye pia ni Mratibu wa Utafiti huo kwa upande wa Tanzania Bara, Theresia Sagamilwa, amesema kuwa tafiti kama hizo zilifanyika nchini mwaka 1990,1995 na 2019 kwa Jiji la Dar es salaam pekee. Utafiti wa Sekta Isiyo Rasmi wa mwaka 2025 ni utafiti wa nne akiwa sasa ni kwa mara ya kwanza unafanyika ukijumuisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naye, Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar ambaye pia ni Mratibu wa utafiti huo kwa upande wa Zanzibar, Rayyan Maalim Kassim, amesema kuwa kwa upande wa Zanzibar Utafiti huo ni wa tatu ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1990, 2013 na 2025.

Ameongeza kuwa taarifa zilizokusanywa kwenye Utafiti huo ni muhimu kwa sababu zinatumika kufahamu ukubwa wa sekta hiyo, na namna gani Serikali inaweza kuboresha sekta hiyo kwa sababu sekta hiyo ni kubwa na inachangia pato kubwa la Taifa.