NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026 Tanzania Inflation Rate April 2026: 4.0 %
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

NBS, OCGS Zaanza Uhariri, Uchakataji Taarifa Utafiti wa Kina wa Shughuli za Biashara 2025
Posted On: 20 May, 2026
NBS, OCGS Zaanza Uhariri, Uchakataji Taarifa Utafiti wa Kina wa Shughuli za Biashara 2025

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar –OCGS zimeanza zoezi la kuhariri na kuchakata taarifa za Utafiti wa Kina wa Shughuli za Biashara 2025 baada ya kukamilika kwa ukusanyaji wa taarifa zake Tanzania Bara na Zanzibar ambalo limeanza tarehe 12 hadi tarehe 24 Mei 2026 katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Kigoma likiwakutanisha wataalam wa Takwimu kutoka pande zote mbili.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mtakwimu Mwandamizi ambaye pia ni Mratibu wa Utafiti huo Kalisto Lugome, amesema kuwa huo unafanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara ya kwanza ambapo awali utafiti huo ulifanywa na Benki ya Dunia - WB mwaka 2023 ambapo ulihusisha mikoa michache.

Mara baada ya kukamilika kwa ukusanyaji wa taarifa kutoka uwandani, timu ya wataalamu tumekutana katika hatua ya kuhariri, kuchakata na kuchambua taarifa hizo kwa ajili ya kuandaa ripoti tatu ambazo ni Tanzania Bara,Tanzania Zanzibar na ripoti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.” Amesema Lugome.

Aidha, ameeleza kuwa utafiti huo umehusisha sekta tisa kati ya sekta 21 zilizopo, huku ukijikita zaidi katika shughuli za kibiashara zinazomilikiwa na sekta binafsi kama vile uzalishaji viwandani, utalii, ujenzi, biashara za jumla na rejereja, Ukarabati wa magari na pikipiki,usafirishaji na uhifadhi.

Ameongeza sekta nyingine ni huduma za maradhi na chakula, habari na mawasiliano, shughuli za kitaaluma, kisayansi na kiufundi, shughuli za kiutawala na huduma saidizi kwa lengo la kufahamu changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.

Ameongeza kuwa matokeo ya utafiti huo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2026 baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa taarifa zote zilizokusanywa.

Pamoja na hayo, Lugome ametoa wito kwa taasisi na Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa timu za watafiti wanaofika katika maeneo yao kwa ajili ya kukusanya taarifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zitasaisaidia Serikali pamoja na Wadau kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo. Pia, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya Takwimu rasmi na ripoti zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo endelevu ya taifa.