NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

Inflation Rate for July, 2026: 4.2% AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

NBS, OCGS Zashirikiana, UNICEF Kuandaa Ripoti ya Umaskini wa Mtoto
Posted On: 13 August, 2026
NBS, OCGS Zashirikiana, UNICEF Kuandaa Ripoti ya Umaskini wa Mtoto

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar – OCGS zimeshiriki mdahalo wa pamoja ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF wenye lengo la kubadilishana uzoefu wa kupima umaskini wa mtoto kwa kutumia methodolojia ya Mbinu ya Makubaliano (Consensual Approach) ambayo itatumia taarifa za utafiti Jumuishi wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania- IHBS 2025.

Akizungumza katika mdahalo huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za UNICEF Osterbay jijini Dar es Salaam tarehe 12 Agosti 2026, Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Kijamii na Demografia kutoka NBS, Elinzuu Nicodemo amesema ripoti hiyo inalenga kuangazia mahitaji ya msingi kwa Watoto.

Nicodemo amefafanua kuwa endapo jamii inatambua kuwa ni hitaji la muhimu, na iwapo kaya inaweza kuyagharamia mahitaji hayo. Hivyo, taarifa hizo zitatumika kupima umasikini wa mtoto kwa kuangalia mahitaji yaliyoainishwa.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa NBS imekamilisha zoezi la kukusanya taarifa za Utafiti wa IHBS 2025 ambao unaopima umasikini wa kaya binafsi. Hivyo, taarifa zilizopatikana zitatumika pia kupima na kuandaa ripoti ya umaskini wa mtoto kwa kutumia methodolojia hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Mkurugenzi wa Utawala na Mipango kutoka OCGS, Abdalla K. Abdalla ameeleza kuwa, kwa mara ya kwanza matokeo ya IHBS yatajumuisha Tanzania nzima jambo ambalo linatoa fursa kupata ushahidi unaowakilisha Taifa kuhusu umasikini wa watoto katika nyanja mbalimbali.

Hivyo, ameishukuru UNICEF kwa kuendelea kufadhili shughuli zinazotekelezwa na Ofisi hizo katika uzalishaji wa Takwimu zinazotegemewa katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

Naye, Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Elke Wisch amesema kuwa hatua hiyo inaonesha nguvu ya ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizo katika kuimarisha upimaji wa umasikini wa watoto nchini Tanzania.

Wisch amesema, kujumuisha mbinu ya Consensual Approach katika Utafiti wa IHBS Tanzania inaweka msingi wa kuzalisha mara kwa mara Takwimu rasmi na bora zaidi ili kusaidia sera na programu zinazolenga kuboresha maisha ya mtoto.

Wadau wengine walioshiriki mdahalo huo ni wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff cha nchini Uingereza, Ofisi ya Takwimu Uganda - UBOS, Ofisi ya Takwimu Brazil pamoja na Wizara za kisekta.