NBS Yakabidhi Machapisho 7,040 Mikoa ya Iringa, Mbeya
Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS imekabidhi nakala za vitabu na machapisho 7,040 ya takwimu rasmi kwa lengo la kuhakikisha Takwimu zinawafikia watumiaji wa takwimu na kuimarisha ufundishaji, ujifunzaji na utafiti katika vyuo mbalimbali na maktaba za mikoa.
Katika Mkoa wa Iringa ni Maktaba ya Mkoa, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Chuo Kikuu cha Iringa, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha, Chuo Kikuu cha Mkwawa, Chuo cha Veta, Chuo cha Afya na Ustawi wa Jamii Iringa na Ofisi ya Meneja Takwimu Mkoa – NBS.
Katika Mkoa wa Mbeya ni Maktaba ya Mkoa, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, Chuo cha Elimu ya Biashara, Taasisi ya Uhasibu Tanzania, (Mbeya health training institute) na Ofisi ya Meneja Takwimu Mkoa - NBS
Nakala hizo zinajumuisha machapisho mbalimbali yanayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikiwemo Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi, Takwimu za Ajira pamoja na taarifa nyingine muhimu za kijamii na kiuchumi.
Aidha, katika kuhakikisha machapisho yana wafikikia na kutumiwa na Taasisi za Serikali, Wadau na Wananchi, NBS imehakikisha machapisho hayo yanapatikana katika mifumo yake ya kidijitali, ikiwemo tovuti rasmi, ili kuwafikia watu wengi zaidi.