NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026 Tanzania Inflation Rate April 2026: 4.0 %
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

Seiya: Uandaaji Wasifu wa Mkoa Kuvutia Wawekezaji
Posted On: 13 May, 2026
Seiya: Uandaaji Wasifu wa Mkoa Kuvutia Wawekezaji

Katibu Tawala Msaidizi (Mipango) Mkoa wa Arusha, Apolinary Seiya amesema uandaaji wa Wasifu wa Kijamii na Kiuchumi wa Mkoa wa Arusha utasaidia kuvutia wawekezaji kwa kutoa taarifa sahihi ya fursa zilizopo mkoani humo.

Seiya ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya uandaaji wa Wasifu wa Kijamii na Kiuchumi wa Mkoa wa Arusha yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tarehe 11 Mei 2026.

Kiongozi huyo amesema kukamilika kwa Wasifu huo, utakuwa msingi wa kusaidia Mkoa wa Arusha kuanza kupima utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Tano wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano pamoja na Dira 2050.

Mafunzo hayo ambayo ni utekelezaji wa Waraka uliotolewa na Waziri Mkuu, ukizitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa Wasifu huo, yameshirikisha wataalamu kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.

Washiriki watapatiwa mafunzo kulingana na Sekta zao ikiwemo Sekta za Ardhi, Mapato, Kilimo, Ufugaji, Maliasili, Utalii na Misitu ambapo mara baada ya mafunzo hayo kukamilika, washiriki watapata nafasi ya kwenda uwandani kukusanya taarifa za kijamii na kiuchumi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya sekta za Serikali na zisizo za Serikali ili kuzalisha Takwimu rasmi zitakazoiwezesha Serikali pamoja na wadau kupanga vema mipango ya maendeleo kutokana na mahitaji yaliyopo.

CHANZO: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.