SG Dkt. Msengwa Ahudhuria Mkutano wa Kikanda wa Takwimu za Kijinsia nchini Kenya
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa hivi karibuni amehudhuria mkutano wa Kikanda uliowakutanisha Wataalam ngazi ya Kiutawala wanaoshughulikia Masuala ya Takwimu zenye mlengo wa kijinsia.
Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uwezeshaji Wanawake (UN Women) umefanyika kwenye Hoteli ya Movenpick, Westland Nairobi nchini Kenya kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 26 Machi, 2026.
Pamoja na mambo mengine, lengo la Mkutano huo lilikuwa kuzindua Ripoti ya Women and Girls Count Phase III ambapo viongozi hao walipata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya uzalishaji na matumizi ya Takwimu zenye mlengo wa kijinsia kutoka nchi zilizo katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
Viongozi hawa walijadiliana kuhusu mafanikio, mafunzo na changamoto wanazokutana nazo katika uzalishaji na matumizi ya Takwimu za Kijinsia, ikijumuisha njia mbalimbali zinazoweza kutumika kuboresha uzalishaji, matumizi na uwasilishaji wa takwimu hizo.