Wataalam NBS Waanza Zoezi la Uchakataji Maoni ya Wadau Maandalizi ya SP Mpya
Wataalam wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS wameanza zoezi la kuchakata maoni ya wadau wa Takwimu nchini kutoka sekta za umma na sekta binafsi baada ya kukamilika kwa zoezi la kupokea maoni ya wadau hao, kwa lengo la kuboresha rasimu ya Mpango Mkakati - SP wa Ofisi hiyo wa mwaka 2026/2027 hadi 2030/2031.
Hatua hiyo inakuja kwa kuwa Mpango Mkakati wa Awali wa NBS unafikia ukomo wake mwezi Juni 2026 ambapo zoezi hilo limeanza tarehe 17 Mei 2026 kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Hoteli ya Corridor Spring mkoani Arusha.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Meneja Mipango na Bajeti, Huzaima Mushi amesema Ofisi hiyo imepikoea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau na kuyafanyia kazi ili kuboresha rasimu mpya ya Mpango Mkakati – SP huo kwani kwa wakati.
Mushi amesema Takwimu ni msingi muhimu katika kupanga mipango ya maendeleo nchini, hivyo NBS kama taasisi ya Serikali ni lazima iwe na Mpango Mkakati ulio hai ili iweze kutekeleza vema na kwa ufanisi majukumu yake.
“Tuna lengo la kupata rasimu mpya ya Strategic Plan (Mpango Mkakati) ambayo itatuongoza vyema katika kipindi chote cha miaka mitano ijayo, hivyo ni vema kufanyia kazi maoni yote ya wadau mbalimbali wa Takwimu, kwani wadau hao ndio watumiaji wa Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kuvutia uwekezaji, utafiti na elimu, kutunga Sera, ugawaji wa rasilimali na kupanga mipango mbalimbali ya Maendeleo ya Nchi.” Amesema Mushi.
Aidha, maoni yanayoendelea kuchakatwa ni pamoja na maoni yaliyo tolewa na Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Watumishi pamoja na maoni ya wadau mbalimbali wa Takwimu yaliyotolewa kwenye kikao cha ukusanyaji wa maoni ya wadau hivi karibuni.