Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Takwimu za Mara kwa Mara

Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutayarisha na kusambaza takwimu rasmi zikiwa ni pamoja na takwimu za mara kwa mara (high-frequency data) kutoka wizara, taasisi za wakala za Serikali. Vilevile, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaratibu Mfumo wa Taifa wa Takwimu kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351.

Takwimu za mara kwa mara ni takwimu zinazotayarishwa kila baada ya: saa, siku, juma au mwezi. Takwimu za mara kwa mara zinajumuisha: viwango vya kubadilisha fedha, mabadiliko katika soko la hisa, mfumuko wa bei, idadi ya watalii walioingia nchini pamoja na uzalishaji wa bidhaa na huduma. Takwimu za mara kwa mara ni muhimu katika kufanya uamuzi wa kisera wenye ushahidi wa kitakwimu kwa wakati na pia ni chanzo muhimu cha kutayarisha modeli za kiuchumi.