MFUMUKO WA BEI WABAKI 4.3%
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Mwezi Septemba, 2026 umebakia kuwa asilimia 4.3 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti, 2026.
Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Mwezi Septemba, 2026 ni sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti, 2026.
Pamoja na kwamba Mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Septemba, 2026 kuwa sawa na wa mwaka ulioishia Mwezi Agosti, 2026, kumekuwa na ongezeko la bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa mwaka ulioishia Mwezi Septemba, 2026 ikilinganishwa na mwaka ulioishia Mwezi Agosti, 2026.
Kwa ujumla, Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia Mwezi Septemba, 2026 umeongezeka hadi asilimia 3.9 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti, 2026.
Mfumuko wa Bei usiojumuisha bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa Mwezi Septemba, 2026 umebakia kuwa asilimia 4.6 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti, 2026.