NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

Inflation Rate for August, 2026: 4.3% AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

NBS Yaendelea Kutoa Elimu Matumizi Takwimu Rasmi Geita
Posted On: 28 September, 2026
NBS Yaendelea Kutoa Elimu Matumizi Takwimu Rasmi Geita

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS inaendelea kutoa elimu kwa taasisi. Wadau pamoja na wananchi kuhusu matumizi ya Takwimu ramsi zinazozalishwa na kusambazwa na Ofisi hiyo kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Kitaifa ya Madini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Maonesho vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombambili, Manispaa ya Geita mkoani Geita.

Matukio katika picha ni wageni waliotembelea kwenye Banda la NBS viwanjani hapo tarehe 25 Septemba 2026, maonesho ambayo yameanza rasmi tarehe 23 Septemba 2026 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 3 Oktoba 2026 yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Madini ni Utajiri, Tuwajibike kwa Pamoja, Kufikia Dira ya Taifa 2050”.

Katika maonesho hayo, NBS inatoa fursa kwa taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, wadau wa maendeleo na wananchi kupata elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya Takwimu rasmi katika kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS inazikaribisha taasisi, wadau na Wananchi  wa Mkoa wa Geita pampoja na maeneo jirani kutembelea Banda hilo ili kupata elimu na kujifunza zaidi kuhusu masuala ya Takwimu na namna Takwimu rasmi zinavyoweza kutumika luleta mabadiliko ya huduma na kiuchumi nchini.